Home / Habari Za Kitaifa

Habari Za Kitaifa

Wanawake 500 kujadili fursa leo

TAKRIBANI wanawake 500 kutoka nchi 25 za Afrika, wanatarajiwa kukutana nchini leo, katika kongamano la kuwakutanisha pamoja wanawake (Africa Reconnect), kwa ajili ya kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo namna ya kujiinua kiuchumi kupitia mapinduzi ya viwanda. Kongamano hilo litakalohudhuriwa na wanawake wa kada mbalimbali wakiwemo wake wa marais, watoa …

Read More »

Maandalizi mradi wa Stiegler’s Gorge yaiva

ZABUNI ya uuzaji wa miti kwenye eneo ambalo litatumika kwa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwenye maporomoko ya Mto Rufi ji ya Stiegler’s Gorge zimefunguliwa jana. Kufunguliwa kwa zabuni hizo kunatokana na muda uliotangazwa wa kimataifa wa siku 21 kukamilika juzi tangu Aprili 25, mwaka huu. Mtendaji Mkuu wa …

Read More »

Tanzanite One sasa kuilipa fidia serikali

KAMPUNI ya uchimbaji madini ya Tanzanite One imekubali kuilipa serikali fi dia pamoja na kodi watakayokubaliana kutokana na dosari zilizokuwepo hapo awali. Makubaliano hayo yalitiwa saini jijini Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Rais John Magufuli, Profesa Palamagamba Kabudi na Mkurugenzi wa Tanzanite One, Faisal Juma. …

Read More »

Kodi mafuta ghafi kuongezwa

SERIKALI imelieleza Bunge kuwa itaongeza kodi kwenye mafuta ghafi yanayoingizwa nchini kutoka asilimia 10 hadi 25. Wizara ya Kilimo pia imewasilisha Wizara ya Fedha na Mipango mapendekezo ya kuboresha mfumo wa kodi na tozo kwa lengo la kuboresha mazingira ya uwekezaji na uendeshaji biashara kwenye shughuli za kilimo. Waziri wa …

Read More »

JPM atoa maagizo 5 mazito mafuta ya kula

RAIS John Magufuli ametoa maagizo matano kwa watendaji wa wizara na idara za serikali, alipofanya ziara ya kushtukiza muda wa saa 6.30 mchana, kufuatilia sakata la mafuta ya kula kwenye Bandari ya Dar es Salaam jana, ikiwemo kuagiza mafuta hayo kutolewa bandarini haraka. Rais Magufuli alitoa maagizo hayo, baada ya …

Read More »

Kilimo kuwa cha kibiashara zaidi

WIZARA ya Kilimo imelieleza Bunge kuwa, mwelekeo wa sekta ya kilimo itakaousimamia kuanzia sasa hadi mwaka 2025 ni kuleta mageuzi ya kilimo kutoka mtazamo wa kilimo cha kujikimu kwenda kwenye mfumo wa kilimo cha kibiashara. Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Charles Tizeba amesema, lengo la mageuzi hayo ni kuhakikisha shughuli …

Read More »

Benki Kuu yaziunganisha benki za TPB na Twiga

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeziunganisha Benki za Twiga na TPB na kuwa benki moja kwa malengo ya kuongeza ufanisi wa taasisi za fedha za kiserikali. Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam leo (Jumatano) na Naibu Gavana wa BOT, Bernard Kibesse huku akieleza dhamira ya kuchukua uamuzi huo ni kuleta …

Read More »

Mshahara wa Waziri ulivyoshikiliwa

MSHAHARA wa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage juzi ulishikiliwa mara kadhaa na wabunge waliokuwa wakionesha ukali wao kuhusu ufufuaji wa viwanda nchini na mradi unganishi wa mchuchuma na Liganga. Aidha, wabunge hao walikuwa wanataka kujua hali na kauli za serikali kuhusu malipo ya fidia kwa wananchi walioacha …

Read More »

Ekari 366 zarasimishwa kwa ‘wavamizi’ Dar

SERIKALI imerasimisha ardhi yenye ekari 366 eneo la Somji iliyopo katika Mtaa wa Dovya, Kata ya Bunju jijini Dar es Salaam kwenda kwa wananchi wa eneo hilo na kuwahakikishia kuwapatia hati halali za umiliki wa eneo hilo. Hatua hiyo inatokana na kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu wa umiliki wa …

Read More »

Mradi wa Stiegler’s Gorge kuanza Julai

WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema kazi ya ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu za maji ya Mto Rufi ji eneo la Stiegler’s Gorge, unatarajiwa kuanza Julai mwaka huu. Dk Kalemani alisema jijini hapa jana kuwa hatua hiyo ya kuanza kwa mradi inatokana na kazi ya tathmini …

Read More »