Home / Habari Za Kitaifa (page 20)

Habari Za Kitaifa

Ndalichako aanika udhaifu Bodi ya Mikopo

SERIKALI imeeleza kwamba matatizo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ni kulipwa kwa wanafunzi hewa, ubadhirifu wa fedha na kuwepo kwa watendaji wanaohusika kuweka fedha za wanafunzi wanne kwa mwanafunzi mmoja. Kadhalika imeeleza tabia ya HESLB kujiona ‘Mungumtu’, kuwaona watoto wa Watanzania kama ni shida …

Read More »

Tanzania kinara malipo mtandaoni

TAASISI ya Trademark East Africa imepongezwa kwa kuiwezesha Tanzania kuwa ndiyo nchi inayoongoza nchi zote za Afrika Mashariki kwa matumizi ya mifumo ya malipo kwa njia ya mtandao, kulipia huduma mbalimbali za kibiashara, hivyo kupunguza gharama za kufanya biashara. Aidha, hatua hiyo imeifanya Tanzania kuwa ni nchi ya mfano wa …

Read More »

Nkurunziza asifia bidhaa za Tanzania

RAIS Pierre Nkurunziza wa Burundi ametembelea maonesho ya kwanza ya biashara ya Tanzania nchini Burundi yanayolenga kuangalia soko pana la bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali kutoka Tanzania na kusifu ubora wa bidhaa hizo. Maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Tempete vilivyopo jijini Bujumbura, yalianza Septemba 28, mwaka huu na yalitarajiwa kukamilika …

Read More »

Waliokula mil 359/- za barabara zawakwama

BODI ya Mfuko wa Barabara imeziamuru halmashauri saba nchini zilizotumia zaidi ya Sh milioni 359.5 zilizotolewa kwa ajili ya kujengea barabara, lakini zikazitumia kununua madawati na kujengea maabara kuzirudisha mara moja katika mfuko huo. Halmashauri hizo ni Karagwe Sh milioni 55.5, Kyerwa Sh milioni 36.8, Ushetu Sh milioni 15.7, Masasi …

Read More »

‘Wazee hatupati huduma bure’

LICHA ya Sera ya Wazee kuelekeza wapatiwe matibabu bure, huduma hizo zimekuwa na changamoto kubwa katika baadhi ya hospitali, vituo vya afya na zahanati nchini. Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika Kongamano la Wazee lililofanyika mjini hapa likiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, Raphael Chandalo kutoka Kasulu …

Read More »

Aliyeondoka Chadema ataka waache kumsakama

ALIYEKUWA diwani wa kata ya Kimandolu kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jijini Arusha ambaye alijiuzulu na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rayson Ngowi amewataka wabunge wa Chadema mkoani Arusha wanaomtuhumu kupokea rushwa wanyamaze kwa kuwa wanachokifanya ni siasa zisizoenda na wakati. Ngowi na diwani wa kata …

Read More »

Waomba kesi za mimba ziwe korti za mwanzo

MWANASHERIA Grace Timoth ameiomba Serikali kuruhusu kesi zinazohusu mimba kwa wanafunzi, kuendeshwa na mahakama za mwanzo, badala ya mahakama za wilaya. Amesema hali hiyo itawaondolea mzigo wazazi na mashahidi kufika kwenye mahakama za wilaya. Amesema kwa sasa watu wengi wamekuwa wakishindwa kufika wilayani, hali inayosababisha kesi nyingi kushindwa kupata ushahidi …

Read More »

Daktari anayetuhumiwa kulewa yamkuta makubwa

WAZIRI wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu amemwelekeza Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Dk Zainab Chaula kumchukulia hatua daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Maswa, Laurent Biyengo aliyedaiwa kushindwa kuingia kazini na kwenda kunywa pombe na kusababisha wagonjwa kutopatiwa huduma. Aidha, Polisi wilayani humo imethibitisha kumkamata …

Read More »

Mikoa mitano vinara mimba za utotoni

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeutaja Mkoa wa Katavi kuwa ndiyo unaoongoza nchini kwa kuwa na tatizo la mimba za utotoni, ambako tatizo hilo lipo kwa takribani asilimia 45. Aidha, imetaja mikoa mingine inayofuatia kwa tatizo hilo, kulingana na asilimia kuwa ni pamoja na Mkoa …

Read More »

Mbwa 400, paka 20 wachanjwa Kahama

HALMASHAURI ya Mji wa Kahama imeadhimisha Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za Wanyama (Tapo) kwa kutoa chanjo kwa mbwa 419 na paka 20. Akizungumza katika maadhimisho hayo mwishoni mwa juma, Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki …

Read More »