Home / Habari Za Kitaifa (page 3)

Habari Za Kitaifa

Bandari wakanusha uvumi vichwa vya treni

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko amekanusha madai kuwa kichwa cha treni ya njia ya kati kilichopata ajali wakati ikienda Kigoma, siku chache zilizopita kuwa ni kimoja kati ya vile vinavyoshikiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Uvumi kuwa kichwa hicho ni kati ya vile vilivyozuiwa …

Read More »

Tanzania yasikitishwa na kauli za Magharibi

MABALOZI wa kigeni wanaofanya kazi nchini Tanzania wametakiwa kutambua mazingira changamani yanayokabili Taifa hili kabla ya kutoa ripoti kwa umma ambazo hawajathibitisha zenye kuchochea mhemko. Kauli hiyo imo katika taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga (pichani) kwa vyombo vya habari …

Read More »

TSN kutangaza fursa za biashara Zanzibar

JUKWAA la fursa ya biashara Zanzibar linaloandaliwa na Kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) lina lengo la kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo katika visiwani humo. Mhariri Mtendaji wa TSN, Dk Jim Yonazi amesema mjini Zanzibar kuwa, jukwaa hilo litaibua fursa zilizopo visiwani humo ambazo hazifahamiki na kwamba, zaidi …

Read More »

28,000 mnada wa Pugu wakalia kuti kavu

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameunda timu ya wataalamu ili kuhakiki uhalali wa nyaraka za wananchi wapatao 28,000 wanaioshi ndani ya eneo na Mnada wa Mifugo wa Kimataifa wa Pugu uliopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam ili kuiwezesha serikali kufanya maamuzi sahihi ya kumaliza mgogoro huo …

Read More »

Mtanzania auawa kinyama Afrika Kusini

WIZARA ya Mambo na Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imethibitisha kifo cha mwanafunzi Mtanzania aliyekuwa akisoma nchini Afrika Kusini. Akizungumza na gazeti hili, Msemaji wa Wizara hiyo, Mindi Kasiga alifafanua kuwa kwa sasa wizara imewasiliana na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ili kubaini undani wa suala hilo. Alisema …

Read More »

Ndalichako atoa miezi 3 mlundikano wanafunzi kumalizwa

SERIKALI imetoa miezi mitatu kwa Maofisa elimu wa mikoa kuhakikisha wanaondoa mlundikano wa wanafunzi madarasani hasa waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichakoalipokuwa akifunga kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya …

Read More »

Laini za simu nchini zafikia milioni 40

LAINI za simu za mikononi zimeongezeka kutoka 2,198 mwaka 1995 hadi kufi kia zaidi ya milioni 40 ilipofi ka Desemba mwaka jana, ambazo zipo mikononi mwa watu na hivyo kuendeleza ustawi wa Watanzania. Katika hatua nyingine, serikali imezindua mfumo wa kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole (biometria), …

Read More »

Wagambia watua kujifunza utoaji haki

JAJI Mkuu wa Jamhuri ya Gambia, Hassan Bubacar Jallow amewasili Tanzania kwa ziara ya kikazi kujifunza na kujipatia uzoefu kuhusu mfumo wa utoaji haki nchini. Atatumia nafasi hiyo kujifunza maboresho mbalimbali yakiwamo ya maslahi ya watumishi yanayoendelea katika Mahakama ya Tanzania na taasisi nyingine za sheria na utoaji haki. Akiwa …

Read More »