Home / Habari Za Kitaifa (page 30)

Habari Za Kitaifa

Mdee asakwa na polisi, kutupwa korokoroni

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Ally Hapi alimeliagiza Jeshi la Polisi wilayani humo kumkamata Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (pichani) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa tuhuma za kutoa lugha za matusi, dhihaka na uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli. Hapi alitoa agizo hilo …

Read More »

Rungu lingine mgodini

BUNGE limepitisha sheria mpya ambayo sasa itatambua haki na dhamana ya serikali katika makinikia ambayo itakuwa ni marufuku kuchenjuliwa nje ya nchi na serikali itashiriki kwa asilimia kuanzia 16 hadi 50 katika shughuli zote za uchimbaji, uchakataji na uchejuaji madini na ununuzi wa hisa katika kampuni ya uchimbaji madini. Aidha, …

Read More »

Wafanyakazi Flyover Tazara Wagoma

WAFANYAKAZI wa kampuni ya LABA Construction Ltd ambao ni vibarua wa kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction company Ltd inayojenga barabara ya juu (Flyover) ya Tazara wamegoma wakishinikiza kuongezwa maslahi yao pamoja na kuitaka kampuni ya Laba kuondoka. Wafanyakazi hao walianza mgomo kuanzia siku ya jana ambapo wanaitaka kampu ni ya …

Read More »

Akamatwa na pembe za ndovu za mil 33/-

POLISI mkoani Morogoro inawashikilia watu watatu akiwamo aliyekutwa na pembe mbili za ndovu zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 33. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei (pichani) alisema mtuhumiwa wa pembe za ndovu alikamatwa Juni 29, mwaka huu saa tano asubuhi katika Kata na Tarafa ya …

Read More »

Bulembo abadili nia, agombea uenyekiti

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdallah Bulembo amechukua fomu juzi mjini hapa kutetea wadhifa wake katika uchaguzi wa ndani ya chama hicho, miezi michache baada ya kutangaza asingewania nafasi hiyo. Bulembo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM alikabidhiwa fomu na Mwenyekiti …

Read More »

TRL yavikataa vichwa vya treni, kurudishwa

KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) imekanusha kuhusika na vichwa 11 vilivyoshushwa na kutelekezwa katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, vichwa hivyo vilivyoshushwa na meli ya Mesina Line tangu wiki iliyopita, na kwamba ni …

Read More »

MAJALIWA:HAKUNA MSAMAHA KWA WANAOUIBIA USHIRIKA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitamsamehe mtu yeyote atakayejihusisha na ubadhilifu wa mali za fedha za Ushirika nchini.   “Kwa Serikali hii ya awamu ya Tano tutachua hatua kali kwa wezi wa mali na fedha za ushirika na tunaendelea kufanya usafi wa wabadhilifu hadi tupate viongozi waadilifu,”.   Waziri …

Read More »

Tizeba: Walioshindwa malengo miradi ya kilimo watupishe

WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba amewataka viongozi wa miradi ya kilimo inayofadhiliwa na serikali na mashirika ya misaada, kuzingatia malengo ya kuanzishwa miradi hiyo ili kuongeza uzalishaji wa chakula nchini, na kwamba kama kuna asiyeweza, ni bora apishe wengine. Akizungumza katika skimu ya umwagiliaji ya Dakawa …

Read More »

Barabara zakarabatiwa Zanzibar

ZANZIBAR imenufaika na mradi ya MIVARF kwa kukarabati barabara zenye urefu wa kilometa 148, zikiwamo zenye urefu wa kilometa 68 za Unguja na 80 Pemba. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Vijana, Kazi na Ajira), Anthony Mavunde alitoa jibu hilo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mgeni Jadi …

Read More »