Home / Habari Za Kitaifa (page 4)

Habari Za Kitaifa

Mkutano wakuu EAC waanza Uganda

MKUTANO wa 19 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umeanza Munyonyo jijini Kampala, Uganda. Marais wa nchi kadhaa wanachama EAC tayari wapo ukumbini akiwemo Rais wa Tanzania, John Magufuli, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, na mwenyeji wao Rais Yoweri …

Read More »

Kenyatta aenda Uganda mkutano wakuu EAC

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameondoka leo kwenda Kampala, Uganda kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Katika uwanja wa ndege jijini Nairobi, Rais Kenyatta ameagwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Fred Matiang’i. Rais John Magufuli aliwasili Kampala jana …

Read More »

Maofisa ardhi wapewa wiki 5 kupima viwanja Dodoma

MAOFISA ardhi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wamepewa wiki tano hadi Machi 31, mwaka huu, kuhakikisha wanapima mashamba na viwanja katika eneo la Ndachi Kata ya Mnadani ili kumaliza mgogoro, uliodumu kwa muda mrefu baina ya wenyeji na wageni. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ametoa muda …

Read More »

Serikali yaikubali bajeti mazishi ya Akwilina

MWANAFUNZI wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) aliyepigwa risasi na kufa katika eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam Februari 16, mwaka huu, Akwilina Maftah (22) anaagwa leo jijini Dar es Salaam na atasafirishwa kwenda kuzikwa Moshi. Serikali na familia ya marehemu wameafikiana kuhusu gharama za mazishi ya msichana …

Read More »

Mwenyekiti, Mwanasheria mbaroni

JESHI la Polisi mkoani Mwanza, kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoani hapa, limemkamata Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Anthony Bahebe. Pia Mwanasheria wa Halmashauri hiyo, Alphonce Sebukoto naye amekamatwa na Jeshi hilo. Viongozi wote hao wanakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya …

Read More »

Hakimu ataka jalada kesi mhasibu Takukuru

HAKIMU Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam , Thomas Simba ameutaka upande wa mashitaka katika kesi inayomkabili Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai kufuatilia jalada la kesi hiyo, lililopo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP). Mbali na …

Read More »

Serikali mbioni kuleta wakala wa maji vijijini

waziri wa kilimo

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa, amesema kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi, Bandari ya Dar es Salaam inatarajia kupata mapato halisi ya Sh bilioni 450. Akichangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu alisema, mpaka robo mwaka kuanzia Julai hadi Septemba kwa mwaka wa fedha …

Read More »

Magufuli azindua kituo cha mafunzo ya kijeshi

Bagamoyo, Tanzania

Rais John Magufuli amezindua Kituo cha Mafunzo Maalumu ya Kijeshi kilichopo Mapinga katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani. Kituo hicho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi la Watu wa China kwa gharama ya Sh bilioni 67.87 na kitatumika kutoa mafunzo ya kijeshi ya kisasa yatakayowawezesha askari kukabiliana na vitisho …

Read More »

NEC Yatangaza Wagombea udiwani kata 10

mkurugenzi wa tume ya uchaguzi tanzania

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza majina 27 ya wagombea udiwani walioteuliwa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuwania nafasi hizo katika kata 10 zitakazofanya Uchaguzi Mdogo Februari 17, mwaka huu. Uchaguzi huo unafanyika katika kata hizo kutokana na baadhi ya madiwani kujiuzulu nyadhifa zao na vifo. Katika uteuzi huo, …

Read More »