Home / Habari za Kimataifa (page 10)

Habari za Kimataifa

Dawa za kuongeza nguvu za kiume zawaponza Zambia

Walazwa wadi ya kipindupindu sababu dawa za kuongeza nguvu Wanaume watatu nchini Zambia wamelazwa kwa makosa katika wadi ya wagonjwa wa kipindupindu baada ya kunywa dawa za asili zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume. Kiongozi wa mkoa, Chanda Kasolo, ameiambia BBC kuwa mara baada ya kunywa dawa hizo, walianza kutapika kitu …

Read More »

Tumbili ‘waumbiwa’ katika maabara ya China

Zhong Zhong na Hua Hua Tumbili wawili wameumbwa katika maabara nchini China, kwa kutumia mbinu sawa na iliyotumiwa kumuumba kondoo maarufu kwa jina Dolly. Shughuli hiyo ambayo huhusisha kiumbe kuumbwa kutoka kwa kiumbe mwingine bila kujamiiana kwa Kiingereza hufahamika kama ‘cloning’. Hatua hiyo imetoa matumaini kwamba huenda teknolojia hiyo ikatumiwa …

Read More »

Nitampa mafao mazuri Robert Mugabe:Mnangagwa

Rais Emmerson Mnangagwa Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, ameiambia BBC kuwa, atampa malipo mazuri ya kustaafu Rais aliyeng`olewa mamlakani Robert Mugabe na mkewe. Amesema kuwa Mugabe ataendelea kupokea mshahara wake na mafao mengine kama kawaida ikiwemo kusafiri katika kiwango cha kwanza kwenye ndege (first class), pamoja na kusafiri kwa …

Read More »

Trump: Palestina iliikosea heshima Marekani

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na rais Donald Trump pembezoni mwa mkutano wa kiuchumi mjini Davos Rais wa Marekani Donald Trump amehoji iwapo mazungumzo ya amani na Israel yataendelea , akiwalaumu Wapalestina. Bwana Trump alisema kuwa taifa la Palestina liliikosea heshima Marekani kufuatia uamuzi wake uliozua utata wa kutambua …

Read More »

Tasnifu ya Udaktari ya Grace Mugabe yatolewa

Grace Mugabe ni mke wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe Nyaraka hiyo yenye kurasa 226, yenye kichwa ‘Mabadiliko ya Mifumo ya jamii na Majukumu ya Familia’ imechapishwa katika tovuti ya chuo kikuu cha Zimbabwe ikiwasilishwa kwa jina la lake Grace Mugabe alilokuwa analitumia kabla ya kuolewa. Hii imetokea wiki …

Read More »

Mashambulio ya Boko Haram kwa takwimu

Wanamgambo wa Boko Haram walianza uasi mnamo 2009 Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema mara kwa mara kuwa wapiganaji jihadi wa Boko Haram wameshinda lakini uchambuzi wa BBC wa mashambulio yao unaonyesha tofuati ndogo. Takwimu zilizokusanywa na BBC Monitoring zinaonyesha kuwa kundi hilo limewaua zaidi ya watu 900 mwaka 2017, …

Read More »