Home / Habari za Kimataifa / Marufuku ya Laptopu na tabiti kuelekea Marekani yatekelezwa

Marufuku ya Laptopu na tabiti kuelekea Marekani yatekelezwa

Mwanaharakati wa Kuwait Thamer Bourashed akiweka laptopu yake ndani ya mzigo kabla ya kuabiri ndege

Marufuku ya laptopu na tabiti katika eneo la kubeba mizigo ya ndege zinazotoka Uturuki na mataifa mengine ya mashariki ya kati na yale ya Afrika Kaskazini imeanza kutekelezwa.

Maafisa wanasema kuwa vifaa hivyo ambavyo ni vikubwa ikilinganishwa na simu aina ya Smartphone havitaruhusiwa katika ndege ya abiria kwa kuwa huenda vinaweza kubeba vilipuzi.

Ni kampuni moja ya ndege pekee inayoruhusu vifaa hivyo kutumika hadi mtu anapoabiri ndege.

Marufuku hiyo inasimamia mataifa manane huku Uingereza ikitoa marufuku kama hiyo vifaa hivyo kutoka kwa mataifa sita.

Kampuni tisa kutoka mataifa manane -Uturuki, Morocco, Jordan, Misri, UAE, Qatar, Saudia na Kuwait zimeathiriwa na marufuku hiyo ya Marekani.

Mataifa hayo huendesha safari 50 za ndege kuelekea Marekani.

Ndege za miliki ya kiarabu UAE hutoa huduma ya kusafirisha mizigo kupitia ndege na meli katika milango ya viwanja vya ndege ili kuwawezesha abiria kutumia vifaa vyao vya kielektroniki baada ya kuiingia katika eneo la kusubiri ndege hadi wanapoingia ndege.

Hiyo inamaanisha kwamba abiria wanaosafiri mara mbili kutoka mataifa mengine kuelekea Marekani kupitia Dubai wanaweza kutumia vifaa hivyo vya kielektroniki katika safari ya kwanza.

Marufuku ya Uingereza inaathiri ndege zote kutoka Misri, Uturuki, Jordan, Saudia, Tunisia na Lebanon.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea mkutano wa mataifa tajiri G7 unaotarajiwa kufanyika nchini Canada

Rais Trump atoa matamko makali Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *