Home / Michezo / Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny ahamia Juventus

Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny ahamia Juventus

Wojciech Szczesny alikaa misimu miwili kwa mkono Roma

Kipa wa Arsenal kutoka Poland Wojciech Szczesny amehamia katika kalbu ya Juventus ya Italia kwa £10m.

Mlinda lango huyo wa miaka 27 alikaa miaka miwili iliyopita kwa mkopo katika klabu ya Roma.

Sasa, ametia saini mkataba wa kudumu wa miaka minne katika mabingwa wa Italia, Juventus.

Raia huyo wa Poland alichezea Roma mechi 38 msimu uliopita na kumaliza mechi 14 bila kufungwa, nyingi za mechi hizo zikiwa katika Serie A.

“Unapofika Juve, ni kwa sababu umeteuliwa. Sikukawia,” anasema Szczesny, ambaye alichezea Arsenal mechi 132 katika kipindi cha miaka minane.

Szczesny atakuwa sasa anashindania lango na Gianluigi Buffon.

Juventus wamesema tayari wamezungumza na Buffon kuhusu hilo.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 29.05.2018: Mahrez anatafutwa na Man City, Mourinho wasiwasi juu ya Gareth Bale

Manchester City wanamtafuta mchezaji wa Algeria Riyad Mahrez msimu ujao Manchester City wanakaribia kukamilisha ununuzi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *