Home / Habari za Kimataifa / Rais Museveni: Sijaugua kwa miaka 31

Rais Museveni: Sijaugua kwa miaka 31

Rais Yoweri Museveni

Mara nyingi kumekuwa na ripoti za kuugua kwa marais, hasa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.

Bwana Buhari amekuwa akipokea matibabu ya ugonjwa ambao haujulikani mjini London tangu mwezi Mei, ambayo ni ziara ya pili anafanya kupata matibabu nchini Uingereza mwaka huu.

Lakini sasa rais wa miaka mingi wa Uganda Yoweri Museveni, amenukuliwa akisema kuwa hajawai kuwa mgonjwa kwa miaka 31.

“Mshasikia kuwa Museveni ameugua au amelazwa hospitalini kwa miaka 31 iliyipota?” aliuliza Museveni.

“Hii ni kwa sababu ninafuata taratibu za kiafya ambazo zimenisaidia kuzuia baadhi ya magonjwa kama haya, mengi ya magonjwa hata yanazuiwa.”

Baadhi ya marais ambao pia wamesafiri ng’ambo kupata matibabu tangu mwaka uliopita ni pamoja na marais wa Angola, Zimbabwe, Benin na Algeria.

Rais wa Zimbabwe ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1980 amekosolewa na wapinzani kwa kuiongoza nchi “kutoka hospitalini” baada ya kufanya ziara ya tatu nchini humo kupata matibabu mwaka huu.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea mkutano wa mataifa tajiri G7 unaotarajiwa kufanyika nchini Canada

Rais Trump atoa matamko makali Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *