Home / Habari za Kimataifa / Hamas na Fatah waingia katika mkataba

Hamas na Fatah waingia katika mkataba

Viongozi wa Palestina katika mkutano wa awali

Msemaji wa kundi la wapiganaji wa Palestina ,Hamas amesema kuwa kundi hilo limeafikiana na kundi pinzani la Fatah kusitisha mzozo wa muongo mmoja kati yao.

Msemaji huyo amesema kuwa maelezo ya makubaliano hayo yatatangazwa katika mkutano na vyombo vya habari mjini Cairo, ambapo awamu ya pili ya mazungumzo ya upatanishi yanaanza siku ya Jumanne.

Hakujakuwa na ithibati yoyote kutoka kwa Fatah.

Mwezi uliopita Hamas lilisema litafutilia mbali kamati ambayo ilisimamia eneo la Gaza na kutoa udhibiti wake kwa serikali inayoungwa mkono na Fatah katika ukanda wa West Bank.

Ramani ya Palestina
Hamas lilichukua udhibti wa Gaza baada ya kuliondoa kwa nguvu kundi la wapiganaji wa Fatah 2007.- mwaka baada ya Hamas kushinda uchanguzi wa Palestina.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Matarajio ya Trump na Kim kukutana yangalipo

Rais wa Marekani Donald Trump na rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un Raisi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *