Home / Habari za Kimataifa / UKRAIN YAKIUKA ONYO LA URUSI NA KUFANYA MAZOEZI YA KIJESHI

UKRAIN YAKIUKA ONYO LA URUSI NA KUFANYA MAZOEZI YA KIJESHI

Ukrain inasema kuwa imekamilisha salama siku ya kwanza kati ya siku mbili za mazoezi ya kurusha makombora juu ya bahari nyeusi magharibi mwa Crimea.

Urusi ambayo ilimega eneo la Crimea imeyataja mazoezi hayo kuwa ya uchokozi na kutishia kudungua makombora hayo.

Lakini leo Alhamisi halmashauri ya usafiri wa anga ya Urusi ilisema kuwa Ukrain imendoa eneo la mazoezi karibu na mpaka.

Afisa wa Ukrain alisema kuwa mazoezi hayo yaliambatana na sheria za kimataifa
Mapema wiki hii Ukrain ilitoa onyo, ikizitaka ndege kuepuka eneo lililo Kaskazini mwa bahari nyeusi siku za Alhamis na Ijumaa.

Mapema mwaka 2014 eneo la Crimea liligeuka na kuwa mzozo mbaya zaidi tangu viishe vita baridi, kufuatia kuondelewe madarakani kwa rais wa Ukrain aliyeipendelea Urusi Viktor Yanukovych.

SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea mkutano wa mataifa tajiri G7 unaotarajiwa kufanyika nchini Canada

Rais Trump atoa matamko makali Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *