Home / Habari Za Kitaifa / RAIS MAGUFULI AKUBALI MKUU WA MAGEREZA KUSITISHA MKATABA.

RAIS MAGUFULI AKUBALI MKUU WA MAGEREZA KUSITISHA MKATABA.

Rais John Magufuli amekubali na kuridhia ombi la kusitisha mkataba na kustaafu kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) John Minja kuanzia leo.

Taarifa ya Ikulu jijini Dar es Salaam imesema Rais Magufuli amempongeza Kamishna Jenerali wa Magereza Mstaafu John Minja kwa utumishi wake na amemtakia maisha mema ya kustaafu.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Kamishna wa Magereza (CP) Dkt. Juma Malewa kuwa Kaimu Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini hadi hapo uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Magereza utakapofanyika.

SOURCE HABARI LEO

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Wanawake 500 kujadili fursa leo

TAKRIBANI wanawake 500 kutoka nchi 25 za Afrika, wanatarajiwa kukutana nchini leo, katika kongamano la …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *