Home / Michezo / Guardiola ataka wachezaji wa ziada kuongezwa

Guardiola ataka wachezaji wa ziada kuongezwa

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa Fifa inafaa kufikiria kuongeza wachezaji wa ziada na kufikia hadi sita ili kukabiliana na tishio la kuwachosha wachezaji.

Shirika la soka duniani Fifa wiki hii lilithibitisha kuwa litaongeza idadi ya timu zinazoshiriki katika kombe la dunia hadi 48 ikiwa na makundi 16 yenye timu tatu.

Guardiola amesema kwa hatua ya kuongeza idadi ya mechi zitakazochezwa itawachokesha wachezaji.

”Wanafikiria kuongeza idadi ya mechi, kwa kweli kutaathiri ubora”, alisema raia huyo wa Uhispania .

”Nazungumza kwa niaba ya wachezaji. Wana haki ya kupumua, na kupumzika ili kufurahia.Wanaongia kwa sasa ni wachezaji watatu pekee, kwa nini isiwe wanne,watano ama hata sita”.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mali U-20 hawatoki kwa Ngorongoro

TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroes, leo itakuwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *