Home / Habari Za Kitaifa / MWANZILISHI WA JAMII FORUMS MAXENCE MELO ASHIKILIWA NA POLISI

MWANZILISHI WA JAMII FORUMS MAXENCE MELO ASHIKILIWA NA POLISI

Mwanzilishi wa mtandao maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla wa Jamii Forums Maxence Melo anashikiliwa na polisi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jamii Forums Melo anashikiliwa kwa kukataa kutoa taarifa za watumiaji wa mtandao huo.

Alitarijiwa kufikishwa mahakamani Jumatano asubuhi lakini wakili wake ameambia BBC hilo halikufanyika.

Badala yake, taarifa zinadokeza huenda akafikishwa kortini Jumanne asubuhi.

Wakili wa Bw Melo anatafakari uwezekano wa kuwasilisha ombi kortini kupinga kuzuiliwa kwa mteja wake kwa zaidi ya saa 24 bila kufikishwa kortini.

Awali, Mwandishi wetu Sammy Awami alizingumza na mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums Mike Mushi na alianza kwa kuelezea mwanzo wa kesi hiyo.

SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Wanawake 500 kujadili fursa leo

TAKRIBANI wanawake 500 kutoka nchi 25 za Afrika, wanatarajiwa kukutana nchini leo, katika kongamano la …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *