Home / Habari za Kimataifa / NDEGE YAANGUKA NA WANAJESHI 92 NCHINI URUSI.

NDEGE YAANGUKA NA WANAJESHI 92 NCHINI URUSI.

Ndege ya kijeshi ya Urusi imeanguka huko Black Sea

Kuna hofu kuwa huenda abiria wote 92 wamefariki baada ya ndege ya jeshi la Urusi waliokuwa wakisafiria kuanguka baharini katika eneo la Black Sea.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi, imesema kuwa imepata mabaki ya ndege hiyo baharibi kilomita moja unusu kutoka Sochi.

Ndege hiyo muundo wa Tupolev-154, ilikuwa na abiria 91, wakiwemo wanajeshi wa Urusi na kikosi cha bendi cha jeshi maarufu kwa jina Alexandrov Ensemble.

Walikuwa wanatazamiwa kupiga mziki wa bendi ya mkesha wa mwaka mpya katika kambi ya jeshi la wanahewa karibu na mpaka na Syria huko mjini Latakia

kikosi cha bendi cha jeshi maarufu kwa jina Alexandrov Ensemble

Ndege hiyi ilipotea katika mitambo ya Rada, muda mfupi baada ya kupaa angani, kutoka kwenye uwanja wa hoteli moja iliyoko maeneo ya Black Sea huko Sochi.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea mkutano wa mataifa tajiri G7 unaotarajiwa kufanyika nchini Canada

Rais Trump atoa matamko makali Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *