Home / Habari Za Kitaifa / KESI YA ‘NDAMA MTOTO WA NG’OMBE’ YAAHILISHWA.

KESI YA ‘NDAMA MTOTO WA NG’OMBE’ YAAHILISHWA.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha kesi ya utakatishaji fedha ya Sh bilioni 1.8 inayomkabili mfanyabiashara Ndama Hussein (44) maarufu kama ‘Ndama mtoto wa Ng’ombe’, hadi Januari 24 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.

Wakili wa Serikali, Leonard Shayo alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa kuwa shauri hilo limeitwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 24 na kuutaka upande wa mashitaka wajitahidi kukamilisha upelelezi haraka.

Mshitakiwa huyo anakabiliwa na makosa sita, manne yakiwa ya kughushi nyaraka, moja la kujipatia fedha kinyume na taratibu na utakatishaji fedha.

SOURCE HABARI LEO.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Wanawake 500 kujadili fursa leo

TAKRIBANI wanawake 500 kutoka nchi 25 za Afrika, wanatarajiwa kukutana nchini leo, katika kongamano la …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *