Home / Habari za Kimataifa / TRUMP KUTEUA JAJI ANAYEPINGA UAVYAJI MIMBA.

TRUMP KUTEUA JAJI ANAYEPINGA UAVYAJI MIMBA.

Maandamano dhidi ya uavyaji mimba nchini Marekani

Makamu wa rais wa Marekani , Mike Pence, ameuambia mkutano wa watu wanaopinga swala la utoaji mimba kuwa rais Trump mwenyewe atamteua jaji wa mahakama ya juu mwenye msimamo mkali dhidi ya tabia ya utoaji mimba.

Sera ya mwanamke kujiamulia kuhusu swala la utoaji mimba iliidhinishwa nchini tangu 1973.

Bw. Pence, akizungumza huko Washington amesema mkondo huo utabadilishwa na utawala mpya uliopo sasa.

Ni hivi majuzi tu ambapo utawala wa Trump ulitangaza kukata ufadhili kwa mashirika yote duniani yanaoshughulika na kutoa huduma za afya ya uzazi ambazo zinajumuisha pia huduma za utoaji mimba.

SOURCE BBC SWAHILI.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea mkutano wa mataifa tajiri G7 unaotarajiwa kufanyika nchini Canada

Rais Trump atoa matamko makali Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *