Home / Michezo / Ancelotti: Arsene Wenger anafaa kupongezwa

Ancelotti: Arsene Wenger anafaa kupongezwa

Arsene Wenger

Mkufunzi wa klabu ya Bayern Munich Carlo Ancelotti amesema kuwa anamuheshimu mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger na akasema kuwa mkufunzi huyo ataweza kujinasua kutoka kwa shutma ambazo zimekuwa zikimkabili hivi majuzi.

Matokeo mabaya katika ligi ya Uingereza yameongeza uvumi kuhusu hatma ya raia huyo wa Ufaransa huku baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wakimtaka aondoke.

Ancelotti anaamini kwamba Wenger anafaa kupongezwa kwa kazi aliyofanya.

”Alijenga kitambulisho na mbinu nzuri ya kusakata soka” ,alisema raia huyo wa Itali.

”Wenge ana uzoefu wa kujua kwamba katika kazi yetu ni swala la kawaida kukosolewa.

Carlo Ancelotti

kwa hilo hana tatizo. Ninaheshimu sana kazi aliyofanya katika klabu ya Arsena”l.

Ancelotti ambaye aliwahi kuifunza Chelsea alikuwa akizungumza kabla ya mechi ya Jumatano ya klabu bingwa ya awamu ya kwanza kati ya timu hizo mbili nchini Ujerumani.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 29.05.2018: Mahrez anatafutwa na Man City, Mourinho wasiwasi juu ya Gareth Bale

Manchester City wanamtafuta mchezaji wa Algeria Riyad Mahrez msimu ujao Manchester City wanakaribia kukamilisha ununuzi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *