Home / Habari za Kimataifa / Kashfa ya mahindi yamfuta kazi waziri Malawi

Kashfa ya mahindi yamfuta kazi waziri Malawi

Mahindi

Waziri wa kilimo nchini Malawi George Chaponda amefutwa kazi kufuatia kashfa ya ufisadi inayoitwa ‘Maizegate’.

Mwezi uliopita Rais Mutharika aliagiza uchunguzi kuhusu agizo la ununuzi wa mahindi yenye thamani ya dola milioni 34.5 kutoka Zambia.

Inadaiwa kuwa kiwango fulani cha mzigo huo kilitoweka mbali na fedha zilizotolewa kununua bidhaa hiyo.

Bwana Chaponda aliambia BBC wiki iliopita kwamba hataondoka afisini hadi atakapopatikana na hatia ya makosa yoyote swala alilokana.

Waziri wa habari Nicolaus Dausi aliambia chombo cha habari cha Reuters kwamba:

”Rais amemuondoa katika baraza la mawaziri mheshimiwa George Chaponda kuwa waziri wa kilimo mara moja baada ya kupatikana na mamilioni ya fedha katika nyumba yake hapo jana’.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea mkutano wa mataifa tajiri G7 unaotarajiwa kufanyika nchini Canada

Rais Trump atoa matamko makali Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *